Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami lijulikanalo kama Saraya al-Quds, limetangaza kuwa limevilenga kwa makombora miji ya Ashdod na Ashkelon kama jibu la jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mamlaka ya ulinzi wa ndani ya Israel siku ya Jumatano ilitangaza kuwa king’ora cha tahadhari kimesikika katika mji wa Ashkelon, hali iliyoashiria uwepo wa shambulio la makombora.
Vyombo vya habari vya Israel vimeeleza madai ya kuyarikisha kombora moja lililokuwa likielekea angani juu ya Ashkelon.
Vyanzo vya habari pia vimeripoti kuwa makundi ya muqawama kutoka Ukanda wa Gaza yametuma kombora moja kuelekea mji wa Ashkelon unaokaliwa kwa mabavu.
Saraya al-Quds imesisitiza kuwa mashambulizi hayo ni sehemu ya kujibu jinai na uvamizi unaoendelea wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.
Your Comment